MBINU HIZI ZITAKUSAIDIA KUFANIKIWA KATIKA MASOMO YAKO:

 

 
 
Tengeneza Ratiba Nzuri ya Masomo:
Tenga muda maalum kila siku wa kusoma na uzingatie kufuata ratiba hiyo. Usikubali ratiba yako ya kusoma kuvurugwa bila sababu za msingi.
 
Tafuta Mahali Penye Utulivu Wakati wa Kusoma:
Chagua mazingira tulivu na ya kukufanya ujisikie vizuri yasiyo na visumbufu ili kuboresha umakini.
 
Tumia Mbinu Shirikishi katika Kusoma kwako:
Badala ya kusoma tu bila kufanyia kazi maarifa unayopata, fanya mazoezi ya kutumia maarifa hayo kikamilifu kwa kuandika ufupisho (summary), kuwafundisha wenzako (peer teaching), au kuunda kadi za kumbukumbu (flash cards)
 
Gawanya Mada Unazosoma katika Vifungu Vinavyoweza Kudhibitiwa:
Gawanya mada kubwa katika sehemu ndogo ndogo, zinazoweza kusomeka kirahisi zaidi ili kuepuka hisia ya kwamba umelemewa na vitu vingi vya kosoma. 
 
Jipe Muda wa Mapumziko:
Chukua dakika kadhaa za mapumziko mafupi kila unapoanza kujihisi uchovu ili kudumisha umakini. 
 
Tumia Mbinu ya Visaidizi Vinavyoonekana:
Tumia michoro, chati, alama, na visaidizi vingine vya kuonekana ili kusaidia kuimarisha ujifunzaji na kufanya dhana ngumu kueleweka kwa urahisi.
 
Jizoeze Kujipima:
Jipime mara kwa mara kupitia maswali, mitihani ya mazoezi, au tathmini ya kibinafsi ili kuimarisha kujifunza na kutambua maeneo ambayo yanahitaji ukazie zaidi.
 
Kuwa na Mpangilio Mzuri:
Weka material (nyenzo) zako za kusoma katika mpangilio mzuri ili kupunguza kupoteza muda kwenye kutafuta nyenzo zako kila wakati unapotaka kusoma.
 
Jitunze na Zingatia kuwa na Afya Bora:
Tunza afya yako kwa kuhakikisha unapata usingizi wa kutosha, kula chakula chenye lishe bora, kunywa maji ya kutosha, na kujishughulisha na shughuli zinazotumia nguvu za mwili kama mazoezi ya viungo na kazi za mikono ili kuuchangamsha mwili.
 
Tafuta Usaidizi pale Unapohitajika:
Usisite kuomba usaidizi kutoka kwa walimu, au wakufunzi, au wanafunzi wenzako, ikiwa unatatizika kuelewa mada, hoja, au somo fulani.

 

Comments