VITENDO VYA KUFUNDISHIA: Kadi za Maswali

 

Mwalimu,
Unaijua mbinu ya kutumia KADI ZA MASWALI katika ufundishaji?
Matumizi sahihi ya Kadi za Maswali yanaweza kuleta ufanisi mzuri sana katika kufundisha na kujifunza.
 
Jinsi ya kuandaa na kutumia Kadi za Maswali:
1. Andaa maswali na majibu yake, kisha andika kila swali kwenye kadi yake upande mmoja wa kadi. Hakikisha maswali yanaeleweka vizuri.
*Kadi zinaweza kuwa ni vipande vya maboksi, karatasi ngumu, kalenda za zamani, n.k.*
 
2. Pangilia Kadi za Maswali kwa njia inayoleta maana ya mtiririko wa kujifunza. Unaweza kuzipanga kulingana na mtiririko wa mada, kiwango cha ugumu, au vigezo vingine vyovyote vinavyofaa.
Kisha tumia kadi hizo kwenye somo kwa kuchagua namna yoyote kati ya hizi;
 
Kwa Mwanafunzi mmoja mmoja: Mwanafunzi anaweza kupitia kadi moja baada ya nyingine na kujibu maswali yaliyomo kwa kuandika majibu kwenye daftari la mazoezi au karatasi.
 
Kwa kutumia Vikundi: Wagawe wanafunzi katika vikundi vidogo vidogo waulizane maswali kwa kutumia kadi za maswali. Kila mwanafunzi katika kikundi apewe jukumu la kufanya. Kama vile; muuliza maswali, mtunza muda, mwandishi wa majibu, mtunza nidhamu, n.k. Muuliza maswali ahakikishe amepata majibu toka kwa kila mshiriki.
 
Kwa kutumia kama Mchezo wa Darasani: Tumia Kadi za Maswali kuwa mchezo wa kufurahisha kwa kujumuisha vipengele kama vile mashindano ya timu au michuano ya pointi. Hii inaongeza ari na motisha wakati wa kujifunza.
 
Tathmini Uelewa: Fuatilia maendeleo na uelewa wa wanafunzi kwa kuangalia jinsi wanavyochangia mawazo na kushiriki katika kujibu maswali.
 
Katika mchakato wowote kati ya hi yohapo juu, wape Wanafunzi majibu uliyokuwa umeandaa mwishoni ili waoanishe majibu yao na ya mwalimu ili kufanya uhakiki.
 
Faida za kutumia Kadi za Maneno:
Kutunza kumbukumbu: Kadi za Maswali zinahitaji wanafunzi kukumbuka kikamilifu mambo waliyojifunza awali na kutoa majibu kutoka kwenye kumbukumbu zao.
 
Kujenga ushirikiano na uwajibikaji: Kadi za Maswali zinachochea wanafunzi kuzungumza, na kushika nafasi mbalimbali katika vikundi na hivyo kukuza ushrikiano na uwajibikaji.
 
Wanafunzi humiliki mchakato wa ujifunzaji: Kwa sehemu kubwa wanafunzi wanajiongoza wenyewe na hivyo kuwa na mamlaka ya kumiliki mchakto wa kujifunza.
 
Kwa ujumla, Kadi za Maswali ni zana rahisi na yenye nguvu ya kukuza ujifunzaji, utunzaji wa kumbukumbu, na ushiriki darasani.
 

Comments

Popular posts from this blog

VITENDO VYA KUFUNDISHIA: Igizo Dhima

MBINU HIZI ZITAKUSAIDIA KUFANIKIWA KATIKA MASOMO YAKO:

SCHOOL LEADERSHIP: Managing Change